Fanya Biashara Kwa Uhuru

Fanya Biashara Kwa Uhuru

Hatua Nne (4) Muhimu za Kuzingatia Kufanya Biashara Tanzania

Ikiwa unataka kuanza biashara Tanzania ni vizuri sana kufahamu mambo unayopaswa kufuata ili kufanya biashara salama na hata uwekezaji wako kuwa na tija.

Hizi ndio hatua nne muhimu za kufuata;

  • Usajili wa biashara
  • Kupata nambari ya mlipa kodi na kulipa kodi
  • Leseni ya biashara na vibali husika
  • Kufungua akaunti ya biashara benki

1. USAJILI WA BIASHARA

Msajili wa biashara zote kisheria hapa kwetu Tanzania ni BRELA (Business Registrations and Licensing Agency). Usajili wa biashara uko wa namna nyingi lakini aina hizi mbili ndio maarufu na hasa ndio maeneo tunayofanya kwa sehemu kubwa;

  • 1.1. Usajili wa jina la biashara binafsi (sole proprietorship) na;
  • 1.2. Usajili wa kampuni yenye mgawanyo wa hisa (limited company).

2. NAMBARI YA MLIPA KODI

Baada ya kusajili biashara, hatua inayofuata ni kupata namba ya mlipa kodi (TIN) kutoka Mamlaka ya Mapato (TRA). Hapa utafanya malipo ya awali ya kodi pamoja na makato 10% kutoka kwenye malipo ya kodi ya chumba cha biashara ikiwa umepanga (Withholding Tax, WHT). Kisha, utapatiwa “tax clearance certificate” hati muhimu inayomaanisha wewe ni mlipa kodi na huna tatizo na Serikali yako kwa upande huo.

Muhimu Kufahamu: kwa sasa mifumo yote, yaani NIDA, BRELA, TRA, TAMISEMI na BANK inasomana! Hivyo Kitambulisho cha Taifa (NIDA) na Nambari yako ya Mlipa Kodi (TIN) ni vitu muhimu sana kwako ikiwa unataka kumiliki Kampuni.

Pia, pindi KAMPUNI inapokuwa imesajiliwa BRELA tu, moja kwa moja namba ya cheti cha usajili wa kampuni ndio inakua TIN ya kampuni. Hivyo, hamtahitaji tena kusajili TIN nyingine kama ilivyokuwa hapo awali.

Vivyo hivyo, Kampuni inawajibika kufanya mchakato wote wa kikodi kupitia “portal” ya TRA mtandaoni ndani ya siku 14. Kinyume na hapo, kampuni itaanza kupigwa penati kana kwamba tayari inafanya kazi. Timu ya Abasasa Business inafanya kazi kwa karibu na ‘directors’ wa kampuni ili kuepuka mzigo huo mzito usio wa lazima!

Abasasa Business Intelligence Team, 2024

3. LESENI YA BIASHARA

Hati ya malipo ya kodi “tax clearance” na TIN yako, pamoja na cheti chako cha usajili wa biashara/kampuni ni nyaraka muhimu zitakazo hitajika katika kukuwezesha kupata leseni ya biashara. Leseni ya biashara inatolewa na Mamlaka ya Jiji/Manispaa ya mahali biashara yako ilipo. Ijapokuwa kuna baadhi ya biashara/uwekezaji utahitaji leseni husika zaidi ya hii; mfano duka la dawa utahitaji leseni kutoka Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA).

4. AKAUNTI YA BIASHARA

Mambo hayo matatu hapo juu pamoja na taarifa nyingine muhimu kuhusu biashara yako zitahitajika, ili kufungua akaunti ya biashara katika benki ile uipendayo. Kubwa, zingatia kufahamu makato husika na faida mbali mbali iwapo utafungua akaunti ya biashara katika benki hio. Ukimaliza haya yote sasa fanya biashara yako kwa uhuru na kufuata malengo yako kwa makini.

Je, ni Wapi Unaweza Kupata Huduma Hizi Zote Kwa Pamoja?

Ni hapa “ABASASA BUSINESS” pekee utapata huduma ya kusajili Kampuni au Jina la Biashara yako kupitia BRELA-Online Registration System (ORS), TIN/Tax Clearance, Leseni ya Biashara, Kufungua Akaunti Benki na kuingia sokoni kifua mbele. Tunaandaa sisi mahitaji yote muhimu (kama vile; Memorandum & Articles of Association) na pia kusimamia mchakato wote hadi kupata ‘certificates’ ndani ya siku 5 tu za kazi. Kwa msaada zaidi wasiliana na Timu ya Abasasa Business, popote pale ulipo! Tupigie/WhatsApp: 0764267098 au bofya hapa kwa maelezo zaidi.

Uswege Nathan

1 Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are makes.