Mpango Biashara Ndio Mpango Mzima!

Mpango Biashara Ndio Mpango Mzima!

Faida Saba (7) za Kuandaa Mpango Biashara

Ni kawaida na imezoeleka kwa walio wengi miongoni mwetu, kuwa mpango biashara ‘business plan” ni muhimu pale tu unapohitaji kuonyesha wadau ili upate mtaji au wakati taasisi za kifedha wanapohitaji kuona ili wajiridhishe kukupatia mkopo. Lakini, dhana hii sio sahihi, kwa sababu mpango biashara “business plan” ni muhimu wakati wote wa uhai wa biashara – yaani kabla na baada ya kuanza biashara. Kwa kutokuzingatia kuandaa mpango biashara, na hasa mpango biashara unaofaa, hupelekea biashara nyingi au miradi kufa pasipo hata kufahamu sababu ya anguko lake.

Mpango Biashara (Business Plan) Maana Yake Nini?

Mpango Biashara ni andiko rasmi linaloonyesha mwelekeo wa biashara kwa ujumla wake. Ni pamoja na malengo, nia ya kufanya biashara hio, maono, masoko, mtaji na upatikanaji wake, na uchambuzi wa matumizi ya mtaji na jinsi faida inavyoweza kupatikana, pamoja na mikakati mbalimbali ya namna ya kuyafikia malengo husika. Kila aina ya biashara inahitaji kuwa na mpango biashara, iwe kubwa au ndogo, inayotaka kuanza na hata ambayo tayari ilishaanza.

Hapa tumekuwekea FAIDA saba (7) za kuandaa mpango biashara “business plan”;

1. Kuimarisha Wazo (Consolidation)

Kuandika MPANGO BIASHARA inakupa kuona kina, kimo, urefu na upana wa wazo la biashara husika. Siku zote unapopata WAZO LA BIASHARA haliji na kila kitu papo hapo, ni lazima kuamua kutafuta na kubaini zaidi. Unapoandaa MPANGO BIASHARA ni MAANDALIZI ya kufanya NDOTO au WAZO lako KUSHIKIKA!

2. Kubaini Fursa Mpya (New Opportunities)

MPANGO BIASHARA unakupa kuona namna ya kuziendea FURSA mpya, zinazopatikana ndani au sambamba na hilo wazo lako. Tasnia (industry) huwa zinaingiliana katika uhalisia wa utekelezaji wake. Mfano: KILIMO na USAFIRISHAJI wa mazao ya kilimo. Hivyo, unapopanga vema biashara yako utabaini FURSA nyingine za upande wako na kuchukua hatua stahiki.

3. Kubaini Wapinzani (Competitors)

Kuandaa MPANGO BIASHARA makini, unakupa kuwatambua watu, taasisi au kampuni zinazofanya kitu sawasawa na wewe unachotaka kufanya. Hii inazaa UBUNIFU, UVUMBUZI na UMAHIRI wa kuandaa BIDHAA BORA na matumizi ya njia mbadala za kukupa kuwa juu ya washindani wako.

4. Kuongeza Shauku (Inner Desire)

Kwa sababu, MPANGO BIASHARA ulioandaliwa kwa umakini, unakupa kuona mbali na FAIDA ya kule unakotaka kufika, kwa hiyo hatua unayopiga kila siku inaongeza maana zaidi kwako na kukupa shauku ya kufanya zaidi na zaidi; hata ikabidi kukesha kwako si tatizo!

5. Kutanua Maono (Enlargement)

Kuwa na MPANGO BIASHARA, inakupa wakati wote mahali pa KUTAZAMA, KUJIKAGUA na KUJIKOSOA. Kwa namna hii unaweza kufanya MAREKEBISHO hata kwa pale ambapo hukifikiri sawasawa hapo awali na kusababisha MAONO yako kupata NGUVU MPYA na kutanuka zaidi.

6. Kupata Pa Kuanzia (Starting Point)

Pasipo kuandaa MPANGO BIASHARA ni ngumu kufahamu namna rahisi zaidi ya kuanza kutekeleza wazo lako! MPANGO BIASHARA rafiki utakupa wepesi wa kuanza biasahara yako (implementation) na kuwa na hatua za wazi za ukuaji unapoendelea hatua kwa hatua.

7. Kufahamu Gharama na Faida (Projections)

Utaweza kufahamu jumla ya gharama au MTAJI (CAPITAL), MCHAKATO wa BIASHARA nzima na MAKISIO ya FAIDA unayoweza kupata kwa MWAKA MZIMA, au kulingana na MSIMU kama BIASHARA yako ni ya MSIMU; kama vile KILIMO.

Njoo Tuyajenge!

Inakubalika kupata msaada wa kitaalamu zaidi ili kupata MPANGO BIASHARA makini. Wasiliana nasi kwa msaada zaidi: ABASASA BUSINESS INTELLIGENCE UNIT, Bofya/WhatsApp: +255 (0) 764 267098

Uswege Nathan

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are makes.